Klabu ya AS Roma na Barcelona walipanga kucheza kwenye mashindano ya Joan Gamper mwaka huu kwenye kipindi cha pre season ambapo walipanga kucheza August 6 kwenye dimba la Camp Nuo na tiketi zilikuwa tayari zishauzwa kwa wingi.

Barcelona leo wametangaza rasmi kwamba AS Roma wamevunja mkataba wa kucheza mechi hiyo lakini hawakuweza kusema sababu iliyopelekea klabu ya Roma kujiondoa kwenye mchezo huo.

AS Roma

“AS Roma wao wenyewe wameamua, pasipo sababu, kujiondoa kwenye makubaliano ya kimkataba kwa pande zote kutocheza tena mchezo wa kombe la Joan Gamper”  waraka wa mashindano ulisema.

Jimbo la Calatan limetoa ujumbe kuwa litaanza hatua haraka za kurudisha pesa za viingilio ndani ya masaa ya 24, na watafanya mchakato wa kutafuta timu nyingine kwa ajiri ya mchezo huo.

Kwa sasa Jimbo la Catalan linajaribu kutafuta haki za kisheria dhidi ya AS Roma kwa kuwasababishia hasara Barcelona na mashabiki wake kwa kujiondoa bila ya sababu za msingi za kuvunja mkataba.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa