Aston Villa Wamsajili Lucas Digne Kutokea Everton

Klabu ya Aston Villa imekamilisha uhamisho wa aliyekuwa nyota wa Everton, Lucas Digne kwa ada ambayo bado haijawekwa wazi.

Staa huyu tayari alionekana kupoteza radha mbele ya Rafael Benitez pale Goodison Park, huku Chelsea na Newcastle United wakitajwa kuhitaji huduma yake.

Sasa Aston Villa ndiyo wameshinda kinyang’anyiro cha saini ya Lucas Digne, akiwa ni mchezaji wa pili kwenye usajili wa dirisha la Januari baada ya PhiliPpe Coutinho aliyewasili kwa mkopo kutoka Barcelona.

Lucas Digne Aston Villa
Lucas Digne, Aston Villa

“Baada ya Lucas kuwepo sokoni tuliikimbilia fursa ya kumsajili. Kumsajil mchezaji kama huyu wa kiwango chake kwenye dirisha la uhamisho la mwezi Januari ni faida kubwa sana kwenye kikosi chetu” – Steven Gerald

Villa wanaaminika kuwa huenda wametumia £25m kukamilisha usajili wa beki huyu mwenye uraia wa Ufaransa, ambaye atavaa jezi namba 27. Mechi yake ya kwanza inaweza kuwa wikiendi hii dhidi ya Manchester United.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe