Timu ya Aston Villa inazidi kupoteza matumaini ya kubaki ndani ya Ligi Kuu England msimu ujao baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa mabingwa Liverpool.

Sadio Mane, nyota wa Liverpool alifungua pazia la kucheka na nyavu dakika ya 70 na msumari wa mwisho ulipachikwa kimiani na Curtis Jones dakika ya 89 kwa pasi ya kichwa ya Mohamed Salah.

Aston Villa, Samatta Mambo Magumu Epl.

Aston Villa, Samatta Mambo Magumu Epl.

Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta alitumia dakika 17 kuitumikia Villa, ambapo aliingia dakika ya 73 akichukua nafasi ya Keinan Davis.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha jumla ya pointi 89 huku Aston Villa ikiwa nafasi ya 18 na pointi zake 27 ikiwa  timu zote zimecheza mechi 33.

Julai 9, Villa ina kazi ya kumenyana na Manchester United inayonolewa na Ole Gunnar Solskjaer ambayo ipo nafasi ya 5 na pointi 55.

51 MAONI

  1. Aston villa wana roho mbaya sana kocha wao hanatakia haangalie sana wachezaji wake hawana ushilikiano ukiangalia mechi yao hawampi pasi mbwana samata wanamuonea wivu

  2. Aston villa awez kumfunga Liverpool nilijua tuu kwasababu Liverpool awez kupelekeshwa na Aston villa ndio mtokeo hayo walio yategemea wakubaliane nayote

  3. Aston villa mambo yashakua magumu kwake, daraja lishamuhusu mtanzania mwenzetu mbwana samatta angelijua hili asingekuja majira haya ya usajili maana sasa ni wakati wake wa kwenda kucheza ligi daraja la kwanza championship na kule ni kugumu Sana hadi upande tena mpambane kweli tumeona timu nyingi zilio shuka daraja hadi Leo hatujaziona tena ligi kuu mfano Qeen park rangers(QPR) hadi Leo tunaisikia tu kwenye bomba kuja kucheza ligi kuu ya england maarufu Kama EPL.

  4. Dah nmesikitika sana juu ya Aston vila kukubali kichapo kutoka kwa Liverpool ila wasikate tamaa waendelee kukaza buti kwani wanaweza wakabadilisha mamb msimu hujao

  5. Sio mbaya samatta atafanya tuangalie champions ship maana kila wanapokutana na timu nyingine wanafungwa tu acha washuke daraja tu

  6. daah Aston Villa anawakati mgumu sana maana anaweza shuka daraja kwa jinsi inavyo onekana.. maana sizani Kama hatoweza kumfunga man u

  7. Aston villa wapo wakati mgumu sana kwa kipindi hichi sana kocha wao anainekana mzembe kidogo kama angekuwa katika timu za Tanzania angeshaondolewa mapema zaidi ya timu tatu alizocheza nazo ameshafungwa na hatujaona mabadiliko ya timu inabidi aondoke sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa