Aston Villa Wameanza Ligi Rasmi

Klabu ya Aston Villa wameanza ligi rasmi baada ya kufanikiwa kupata ushindi mnono wa mabao manne kwa bila dhidi ya klabu ya Everton katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Aston Villa chini ya kocha Unai Emery walianza ligi vibaya wikiendi iliyomalizika baada ya kufungwa na klabu ya Newcastle, Lakini leo wameonekana kua imara na kuweza kuibuka na ushindi wakiwa katika dimba lao la nyumbani.aston villaVijana wa Unai Emery walionekana kuitawala mechi kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo ambapo walikua wakitandaza soka safi, Ambapo mapema dakika ya 18 ya mchezo John McGinn kuipatia klabu yake uongozi na dakika ya 24 ya mchezo Douglas Luiz kufunga bao la pili na kuwafanya Villa kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili kwa bila.

Kipindi cha pili kilianza Villa wakiwa bado wanaonekana kuendelea kuutawala mchezo na kutengeneza nafasi mara kwa mara na mnamo dakika ya 51 tu Leon Bailey anaongeza bao la tatu kabla ya Jhon Duran dakika ya 75 kufunga bao la nne na kuhitimisha karamu ya mabao.aston villaKlabu ya Aston Villa sasa wamerudi kwenye njia ya ushindi baada ya kupigwa katika mchezo wa kwanza, Lakini pia klabu hiyo ni moja ya vilabu vinavyotarajiwa kufanya vizuri msimu huu kutokana na usajili mzuri walioufanya.

Acha ujumbe