Aston Villa ya Unai ni Vichapo Tu

Klabu ya Aston Villa chini ya kocha Unai Emery kimekua na matokeo mazuri sana ambapo leo wamefanikiwa kuifunga klabu ya Westham United kwa jumla ya mabao manne kwa moja katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Mchezao huo uliopigwa katika dimba la Villa Park jioni ya leo ulishuhudia vijana wa David Moyes wakikubali adhabu kali kutoka kwa Aston Villa ya Unai Emery cha mabao manne.aston VillaMchezo huo ambao ulikua una kasi kuanzia dakika ya kwanza mpaka dakika ya mwisho ulishuhudia Villa wakianza kupata bao kupitia kwa kiungo wake raia wa kimataifa wa Brazil dakika ya 30 ya mchezo ambao uliwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi vilevile na Westham wakionekana wanahitaji kupata goli la kusawazisha, Lakini ni Dougals Luiz aliipatia Aston Villa bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya beki Konsa kufanyiwa mazambi.aston VillaWestham walipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Jarrod Bowen dakika ya 56 ya mchezo kabla ya Ollie Watkins na Leon Bailey kuifungia Villa bao la tatu na la nne na kufanya kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa moja.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.