Klabu ya Aston Villa imeendelea ilipoishia wikiendi iliyomalizika baada ya kufanikiwa kuifunga klabu ya Brighton and Hove Albion mabao mawili kwa moja katika mchezo uliopigwa katika dimba la The American Express Community.

Alexis McAllister alifanikiwa kuwapatia Brighton bao la mapema kabisa kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Dany Ings kuisawazishia Aston Vila na matokeo kua bao moja kwa moja mpaka mapumziko.aston villaVijana wa Unai Emery walirudi kipindi cha pili wakitafuta alama tatu na mshambuliaji Dany Ings afanikiwa kufunga bao dakika ya 54 ya mchezo na matokeo kua mbili kwa moja wageni wakiongoza huku mechi ikiendelea kua ya kutafutana kwa kipindi kirefu.

Klabu ya Brighton walipambana kutafuta bao kwa uchu mkubwa baada ya kufungwa bao la pili lakini vijana Villa walikua makini kwa kiwango kikubwa kulinda bao lao na mpaka mchezo unamalizika klabu hiyo ilifanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu.aston villaHuu unakua ushindi wa pili mfululizo kwa Aston Villa baada ya kuifunga Manchester United wikiendi iliyopita na leo wanapata alama tatu ugenini, Huku klabu hiyo inafanikiwa kupanda hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kufikisha alama 18.

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa