Aston Villa Yakamilisha dili la Barrenechea

Klabu ya Aston Villa imefanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo ambaye alikua anakipiga klabu ya Juventus raia wa kimataifa wa Argentina Enzo Barrenechea.

Klabu ya Aston Villa wanampata mchezaji Enzo Barrenechea katika dili ambalo lilimuhusisha kiungo wa kimataifa wa Brazil Douglas Luiz ambaye amejiunga na klabu ya Juventus, Kiungo huyo inafahamika mpaka sasa ameshakamilisha vipimo vya afya ambavyo ndani ya Villa.aston villaKiungo Douglas Luiz amefanufaisha Aston Villa kwani wamefanikiwa kupata kiasi cha fedha kutoka kwa klabu ya Juventus, Lakini pia wamepata wachezaji wawili kutoka klabu ya Juventus ambao ni Enzo Barrenechea pamoja na Samuel Illing.

Kuelekea msimu ujao ambapo klabu ya Aston Villa itashiriki ligi ya mabingwa ulaya hivo wanahitaji kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu huo husika, Hivo klabu hiyo imeongeza wachezaji watatu mpaka sasa ambao ni Enzo Barrenechea, Samuel Illing, pamoja na Ian Maatsen.

Acha ujumbe