Ateba Atamba Kuifunga Yanga

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Lionel Ateba raia wa kimataifa wa Cameroon amesema hana hofu na mabeki wa klabu ya Yanga ila anachojua yeye atafunga mchezo huo na klabu yake ya Simba itashinda mchezo wa Derby.

Mshambuliaji Ateba ambaye amejiunga na klabu ya Simba mwishoni mwa dirisha kubwa la usajili lililopita ameonesha hali ya kujiamini kwa kiwango kikubwa kuelekea mchezo ambao huvuta hisia za watu wengi nchini mchezo wa Dery ya Kariakoo, Hii inatokana na kauli yake ambaye ameitoa kuelekea mchezo huo mkubwa zaidi Afrika mashariki.ateba“Sitaki kujua Yanga wana Mabeki wazuri, sitaki kujua kuwa wana ulinzi mzuri, sitaki kujua wana Beki sijui anaitwa Sergio Ramos, kwanza sitaki hata kujua majina yao ila nina uhakika nitaingia uwanjani kwenye derby na nitawafunga Yanga na Simba tutashinda, sitaki kujua wana Beki wa aina gani”

Maneno ya mshambuliaji Ateba yanasubiriwa kwa hamu kutimia kwani kwa miaka ya karibuni atakua mchezaji wa pili kutimiza ahadi yake aliyoiweka kuelekea mchezo wa Simba na Yanga, Kwani Mrisho Khalfan Ngassa aliwahi kuahidi mwaka 2013 lazima aifunge Simba na asipofanya hivo nyumba yake ichomwe moto na kwa bahati nzuri alitimiza alichoahidi.

Acha ujumbe