Atletico Madrid wanaripotiwa kuwa tayari kumuuza mshambuliaji wao Joao Felix kwenda Manchester City msimu ujao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa na kipindi kigumu kuonesha ubora wake mbele ya nyavu msimu huu, akifunga mara tatu pekee kwenye mechi 18 katika michuano yote.
Hata hivyo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno anaaminika kupendwa na meneja wa City Pep Guardiola, ambaye angependa kumvuta fowadi huyo kwenye Ligi ya Premia.
Kwa mujibu wa taarifa toka Ureno, kupitia Sport Witness, Atletico wana nia ya kumuuza Felix ili kuwasaidia kumnunua mshambuliaji wa Benfica Darwin Nunez kwa pesa nyingi.
Ripoti hiyo pia inasema kwamba uwezekano wowote wa kuhamishwa kwa Felix kwenye Uwanja wa Etihad utakuwa “mchakato ambao unapaswa kubadilika mwishoni mwa msimu tu”.
Tangu kuwasili Atletico kutoka Benfica kwa takribani pauni milioni 113 msimu wa joto wa 2019, Felix amefunga mabao 22 na kutoa asisti 11 katika mechi 94 alizocheza na kikosi cha Diego Simeone.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA