Aubameyang Ahitajika Saudi Arabia

Klabu ya kutokea nchini Saudi Arabia Al Nassr wamepeleka offs ya kutaka kumsajiri nyota wa klabu ya Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang kwa mkopo, ambaye kwa sasa anaendelea na vipimo baada ya kutoka kwenye michuano ya AFCON.

Mshambuliaji huyo kutoka Gabon Aubameyang amerudishwa kwenye klabu yake siku ya jumatatu pasipo kucheza mchezo hata mmoja yeye na Mario Lemina, baada ya kukutwa na maambukizi ya Uviko-19, huku Aubameyang akikutwa na matatizo ya moyo.

Aubameyang

Pierre-Emerick amebakisha miezi 18 kwenye mkataba wake na washika bunduki wa london, pia hajacheza mchezo wowote tokea December 6 kabla ya kuondoka kwenda kwenye mashindano ya AFCON, hakuwa na mawasiliano mazuri na klabu yake ilipelekea hadi kuvuliwa kitambaa cha unahodha kutokana na matatizo ya kinidhamu.

Klabu iliyopeleka offa ya kumuhitaji Pierre-Emerick kwa mkopo inaotoka nchini Saudi Arabia, Al Nassr iko nafasi ya tatu kwenye ligi kuu ya nchini humo, pia mfungaji bora wa mashindano ya AFCON mkameruni Vincent Aboubakar ni mmoja wa wachezaji wa klabu hiyo.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe