Arsenal wanaendelea kutaabika kwa kupata matokeo mabaya kwenye EPL. Kuelekea mchezo wa robo fainali ya Carabao Cup, Aubameyang atakosekana kwenye mchezo huo.
Arsenal watawakaribisha Manchester City katika dimba la Emirate Stadium siku ya Jumanne usiku katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya Carabao Cup.
Timu hizi zinakutana kwa mara nyingine mwaka huu zikiwa ni siku chache tangu walipocheza mchezo wa fainali ya FA Cup na Arsenal kuibuka kidedea. Ulikuwa ni wakati wa neema kwa Arsenal baada ya kubeba taji la FA, Community Shield na nahodha wao – Pierre -Emerick Aubameyang akasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Tangu walipocheza mchezo wa mwisho, maisha yamebadilika sana kwa vilabu vyote viwili. City amekuwa na matokeo ya kupanda na kushuka wakiwa nafasi ya 7 kwenye msimamo wa EPL.

Aubameyang anaiongoza Arsenal ambayo wameendelea kuwa na matokeo mabovu tangu kuanza kwa msimu huu na sasa wanashikilia nafasi ya 15 kwenye msimamo wa EPL wakiwa na pointi 14 katika michezo 14 waliyocheza mpaka sasa.
Kuelekea mchezo wa Carabao Cup, Mikel Arteta amethibitisha kukosekana kwa Aubameyang ambapo atakuwa anakosekana kwa mara ya pili mfululizo (hakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Everton wikiendi iliyopita).
“Auba alikuwa anajisikia vizuri zaidi jana kuliko siku mbili zilizopita. Atafanyiwa tena vipimo siku chache zijazo, baada ya hapo tutaona atachukua muda gani kurejea kikosini.
“Tunajua anaumuhimu kiasi gani kwetu na anayabeba majukumu hayo na anajitahidi kurejea kwenye ubora wake mapema awezavyo. Auba hayupo tayari kwa mchezo wa kesho, huo ni uhalisia.
“Kesho hatocheza, tutaangalia nani anapatikana kwasababu bado tunamashaka na baadhi ya sehemu zingine pia. Tunahitaji kupata muunganiko wa timu yenye ushindani kwa sababu tunajua viwango walivyonavyo City na tunahitaji kushinda mchezo wa kesho.” Alisema Arteta.
Kukosekana kwa Auba pengine kutamlazimu Arteta kupanga kikosi chenye wachezaji chipukizi wengi ili kuendana na kasi ya mechi zinazofuata kuelekea mwezi Januari 2021.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???
Hopemwaikuka
Get well soon Auba
Dorophina
Arsenal sijui wanakwama wap
Adelta
Arsenal wanatakiwa waongeze juhudi ili waweze kurejea kwenye kiwango
aisha
Arsenal msimu huu sijui inakuaje
Issa
Auba ni moto
Shakila mrope
Du ni mbona hatari
Sarah
Arsenal cjui tatizo nn tena
Lydia Emmanuel Magoti
Duu sio poa
samiah
Sio sawa
Saupha mohamed
Dhuuu nomaa
Latifa juma mohamed
Arsenal msimu huu sijui inakuaje
Flomena
Good news
Ernest Kimeru
Pigo kwa Arteta
Tatu
Pigo kwa arsenal
warda
Ndo hivyo tena haina jinsi