Pierre Aubameyang alihuzunishwa kuona Thomas Tuchel akifukuzwa Chelsea lakini mshambuliaji huyo tayari anafurahia maisha chini ya Graham Potter.

 

Aubameyang: Potter Anaweza Kurejesha Kiwango Changu

Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal (33) amevumilia kipindi kigumu tangu ajiunge na The Blues kutoka Barcelona siku ya mwisho ya uhamisho ili kuungana na Tuchel kufuatia muda wao wa pamoja huko Borrusia Dortmund.

Lakini alipata kucheza mechi moja tu akiwa na kocha wake huyo wa zamani mara moja huku tuu huku wakipata kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Dinamo Zagreb kwenye ligi ya Mabingwa mnamo Septemba 6,ambapo mechi hiyo ilifanya Mjerumani hiyo kufukuzwa.

Tuchel aliondolewa asubuhi iliyofuata na nafasi yake kuchukuliwa haraka na Potter, ambaye alimpa Aubameyang mwanzo wake wa pili katika klabu hiyo katika sare ya 1-1 na FC Salzburg Jumatano iliyopita uwanja wa Stamford Bridge.

Akitafakari matukio ya hivi majuzi, Auba alisema: “Zimekuwa wiki za ajabu kwetu sote nadhani, sio mimi tu. Hiyo ni sehemu ya maisha. “Kila mtu anajua uhusiano niliokuwa nao na Tuchel. Inasikitisha mtu anapoondoka kwenye klabu lakini hii ni soka, inapaswa kuzoea haraka nyakati tofauti katika msimu.

 

Aubameyang: Potter Anaweza Kurejesha Kiwango Changu

Aubameyang anafurahishwa na kile anachokiona hadi sasa ambapo akimzungumzia meneja wake mpya alisema; “Ni mtu mzuri sana.”Ana tabia nzuri sana tutajaribu kujifunza naye na kushinda haraka iwezekanavyo. Itakuwa rahisi kubadilika. Mawazo yake yako wazi sana.”

Auba amecheza akiwa amevaa maski usoni katika mechi zake zote mbili ndani ya Chelsea ili kulinda taya lake lililovunjika. Haionekani kuathiri uchezaji wake lakini mchezaji huyo wa Kimataifa wa Gabon anakiri kuwa bado anafanya kazi ya ziada kuwa fiti kamili.

 

Aubameyang: Potter Anaweza Kurejesha Kiwango Changu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa