Avram Glazer: Mara Zote Tumekuwa Tukitumia Pesa

Avram Glazer amekubali kuwa Manchester United imekuwa na kipindi kigumu msimu huu lakini ameitetea familia yake ambayo ndio wamiliki wa klabu hiyo kuwa wamekuwa wakitumia pesa kufanya maboresho mara kwa mara.

Familia ya Glazer imeimiliki klabu ya Manchester United  kwa miaka 17 sasa lakini tokea waanze kuimiliki wamekuwa wakipingwa vikali na mashabiki wa klabu hiyo, na siku za kuribuni kumekuwa na maandamano ya mara kwa mara ya kutaka familia hiyo iachane na klabu hiyo.

Avram Glazer,wakati akifanyiwa mahojiano na skysports alisema, “ni msimu unaokatisha tamaa kwa kila mmoja wetu na tunaenda kufanya kazi kwa juhudi ili kufanya msimu unaokuja kuwa bora kwetu.”

Alipoulizwa kuhusu uwekezaji kwa msimu ujao kuanzia majira ya kiangazi mwenyekiti mwenza Avram Glazer aliongezea, “Mara zote tumekuwa tukitumia pesa zinazohitajika kununua wachezaji wapya.”

Na alipoulizwa kuhusu kocha mpya ambaye ameanza kazi rasmi leo Jumatatu Erik Ten Hag kuhusu kuipa mafanikio klabu hiyo alijibu, “ndio maana tumemwajiri, tunajua atafanya kazi vizuri.”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe