UONGOZI wa Azam FC umefunguka kuwa wataendelea kushusha vifaa vyao na kuachana na baadhi ya wachezaji ambao wamemalizana nao.

Azam tayari wamewatambulisha wachezaji watano wapya kwa ajili ya kuimarisha kikosi kwa msimu ujao na kuachana na nyota wao wanne.

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ amesema kuwa “Tunaendelea na utambulisho wa wachezaji ambao watakuwepo kwenye kikosi chetu kwa msimu ujao lengo ni kuboresha zaidi kikosi chetu.

“Katika hilo pia tutaendelea kuwatangaza wachezaji ambao tutawaacha na kuwatakia kheri kwani tayari tumeachana nao wanne ila inategemea na makubaliano.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa