Azam Fc Yaipasua Yanga Chamazi

Baada ya kucheza michezo nane bila kupoteza wala kuruhusu goli hatimae klabu ya Yanga leo imepoteza mchezo mbele ya klabu ya Azam Fc kunako ligi kuu ya NBC baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila.

Azam Fc ambao wamekua kwenye kiwango bora siku za hivi karibuni wamefanikiwa kuizuia Yanga kushinda michezo tisa mfululizo ya ligi kuu ya NBC, Ambapo wameweza kuchomoza kwa ushindi wa goli moja kwa bila bao lililowekwa kimiani na mshambuliaji Djibril Sillah dakika ya 33 ya mchezo kuelekea mapumziko.Kipindi cha pili Yanga licha ya kua pungufu walionekana kua na uchu wa kutaka kusawazisha goli walilotanguliwa kwani kipindi kirefu cha mchezo walionekana kutawala mchezo, Lakini Azam waliendelea kuhakikisha wanaimarisha ulinzi kwenye lango lao na kutoruhusu goli na kuwafanya kuondoka na alama tatu muhimu leo.

Ikumbukwe mchezo wa mwisho ambao klabu ya Yanga walipoteza kwenye ligi kuu ya NBC ilikua dhidi ya klabu ya Azam Fc na Yanga walishinda michezo mingi baada ya hapo, Lakini leo tena walewale waliowafunga mara ya mwisho wameshinda tena mbele ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya NBC.azam fcYanga walicheza pungufu kwa takribani dakika 68 za mchezo ambapo mnamo dakika ya 22 beki wake mahiri alimfanyia madhambi mshambuliaji wa matajiri wa jiji la Dar-es-salaam Nassor Saaduni ambapo ilipekea kuoneshwa kadi nyekundu na kuwaacha wenzake wakicheza pungufu kwa muda mwingi wa mchezo.

Acha ujumbe