Kikosi cha Azam FC kinatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya TP Mazembe kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa raundi ya kwanza ya michuano ya Shirikisho barani Afrika.

 

Azam kujipima na Wacongo

 

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ amesema “Kikosi kinaendelea kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali ya mashindano ya Shirikisho barani Afrika”.

“Kikosi kitaondoka Dar Septemba 22 kuelekea Zambia ambapo tarehe 23 watacheza mchezo huo wa kirafiki na Septemba 24 watarejea Dar kwa ajili ya kujiandaa na sehemu inayofuata ya michezo ya ligi dhidi ya Tanzania Prisons na Singida Big Stars na baadae ule wa michuano ya kimataifa dhidi ya Al Akhdar ya nchini Libya.

“Kocha anatumia muda huu mfupi wa mapumziko kwa ajili ya kuhakikisha anapata nafasi ya kukijua vizuri kikosi chake na kukiimarisha zaidi.”

 

Azam kujipima na Wacongo

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa