UONGOZI wa Azam umeweka wazi kuwa unatarajia kuondoka nchini Julai 22, mwaka huu kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi yao ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Preseason’ ambayo inatarajiwa kuwa ya muda wa siku 20 ambazo ni sawa na masaa 480.

 

Usajili Azam

Kambi hiyo ya Azam inatarajiwa kuwa sehemu ya maandalizi ya timu hiyo ambayo pamoja na mashindano mengine itakayoshiriki, inajiandaa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kambi hiyo pia inatarajiwa kuhusisha wachezaji wote ambao wamesajiliwa na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao. Mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith alisema:

“Baada ya kukamilisha usajili wetu kwa zaidi ya asilimia 90, kwa sasa tunafanya maandalizi ya mwisho ya kambi yetu ya maandalizi ya kabla ya msimu ambayo inatarajiwa kuwa katika mji wa El Gouna nchini Misri.

“Kikosi kinatarajiwa kuanza kambi ya awali Julai 18, mwaka huu hapa nchini kabla ya kuondokia Julai 22, mwaka huu kwenda Misri, ambapo tutakuwa na kambi ya siku 20 kujiandaa na mashindano mbalimbali ambayo tutashiriki msimu ujao, hususani tageti yetu kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa