Klabu ya Azam FC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mlinzi wa kushoto, Edward Charles Manyama kutoka katika klabu ya Ruvu Shooting.

Manyama amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya wanalamba lamba yenye makao yake Chamazi Dar es Saalam.

Awali klabu ya wekundu wa msimbazi walihusishwa na beki huyo kitasa huku tetesi zikienea kwamba amemwaga wino katika vigogo hao wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.

“Beki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Manyama, amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Azam FC kuanzia msimu ujao 2021/22 hadi 2023/24.
“Hii ni baada ya kufikia makubaliano na klabu yake ya Ruvu Shooting.” ilisomeka taarifa katika ukurasa wa klabu ya Azam FC.

WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa