Baada ya kukubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru na wana Kino Boys, KMC, vinara wa Ligi Kuu Bara Azam FC wameweka wazi kwamba watapambana kusepa na pointi tatu mbele ya Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, saa 1:00 usiku, Novemba 25.


Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 25 na mabao yake 18 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 25 ikiwa imefunga mabao 13.

Mshindi kwenye mchezo huu atajijengea ufalme nafasi ya kwanza huku ikiwa itatokea sare basi Azam FC itabaki kileleni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa walipambana kadri wanavyoweza mbele ya KMC Novemba 21 ila bahati haikuwa yao kwa upande wa matokeo.

“Huwa tunapambana siku zote kusaka ushindi ila haikuwa bahati yetu mbele ya KMC licha ya wachezaji kuonyesha juhudi.

“Tunarudi tena Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku haitakuwa kazi nyepesi ila tutapambana kupata pointi tatu mbele ya wapinzani wetu.

“Hakuna kingine ambacho kinahitajika ndani ya uwanja zaidi ya timu kupata pointi tatu, maandalizi yapo vizuri na kikosi kipo na morali, mashabiki watupe sapoti,” amesema.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI


21 MAONI

  1. Hayoo maneno tu matokeo iwanjani ingawa wahenga wamasema ukitaka kumshinda adui lazima utazame uzaifu wake hivyo tungoje dk 90 kwa refa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa