MVP wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 Aziz Ki ameweka wazi kuwa kila baada ya mchezo mmoja kinachofuata ni maandalizi kwa mchezo ujao ndani ya uwanja.
Ikumbukwe kwamba Yanga iliweka kambi Afrika Kusini ambapo ilialikwa kwenye mashindano maalumu ilitwaa Kombe la Toyota kwa ushindi wa mabao 4-0 baada ya dakika 90.
Katika mchezo huo Aziz alifunga mabao mawili, Clement Mzize alifunga bao moja na Prince Dube yeye alifunga bao moja la ufunguzi kwenye mchezo huo.
Agosti 4 2024 Yanga ilikuwa ni Wiki ya Wananchi ilipocheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Red Arrows ikapata ushindi wa mabao 2-1 na Aziz Ki alifunga bao moja kwenye mchezo huo.