Baba wa Emiliano Sala Naye Aaga Dunia

Baba wa aliyekuwa nyota wa Ligi Kuu ya Uingereza Emiliano Sala, ambaye pia alifariki kwenye ajali ya ndege, ameaga dunia miezi mitatu baada ya mwanae.

Mr. Horacio Sala alikuwa na umri wa miaka 58, alipatwa na shinikizo la moyo na kufariki kabla ya madaktari kufika nyumbaniu kwake kwa ajili ya huduma.

Baba wa Emiliano Sala Naye Aaga Dunia
Horacio Sala

Mwanae Emiliano Sala, lifariki mapema mwaka huu akiwa kwenye safari kuelekea Cardiff akitokea klabu ya Ufaransa ya Nantes baada aya ndege aliyokuwa akisafiria kuanguka baharini.

Ikiwa ni pigo kubwa jingine kwa familia ya Sala, klabu ya Cardiff imetoa salamu zake za pole kwa jamaa na familia ambao wameguswa na msiba huo.

Mzee Sala ambaye ni baba wa watoto watatu alikuwa katika harakati za kutafuta haki ya mwanawe aliyefariki kwenye ajali. Mzee huyu alikuwa anasisitiza wana usalama na vyombo vya habari kuchunguza suala la mwanae kwa undani zaidi waweze kutambua kwa nini ndege hiyo ndogo ilianguka.

Wapumzike kwa amani baba na mwanawe Sala.

3 Komentara

    Jaman taarifa za huzuni sana poleni wana michezo wote#meridianbettz

    Jibu

    Duu tarifa zakusikitisha Sana mungu ampumzishe mahara pema pepon

    Jibu

    Ri p Salah

    Jibu

Acha ujumbe