Baba wa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Luiz Diaz ameachiwa baada ya kushikiliwa na vikundi vya kihalifu huko nchini Colombia kwa takribani siku kumi na mbili.
Baba wa Luiz Diaz alikua ameshikiliwa na vikundi vya kihalifu nchini Colombia na leo ameachiwa na yupo kwenye mikono ya polisi jambo ambalo limekua la faraja kwa mshambuliaji.Baada ya kutekwa kwa Baba wa mchezaji huyo ilimfanya mchezaji huyo kukosekana katika michezo miwili ya klabu ya Liverpool, Lakini baada ya Baba wa mshambuliaji huyo kuachiwa ni wazi mchezaji huyo atarudi uwanjani na kucheza kwa utulivu.
Klabu ya Liverpool itarejea dimbani kukipiga kwenye michuano ya Uefa Europa League na mshambuliaji Luiz Diaz atakuwepo, Huku akicheza mchezo wake wa leo akiwa na amani kwakua mzazi wake yupo huru kwasasa.