“Bado Nafasi Tunayo!” – United

Baada ya kupoteza mechi yao ya awali dhidi ya Barcelona, klabu ya Manchester United bado wanayo nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo endapo watafanya kile kilichowatokea PSG kwa kusoma mahitaji ya mchezo huo na kufanya makubwa zaidi ili kulinda nafasi yao.

United watakuwa na safari ya kwenda Camp Nou ambao ni uwanja mgumu kuchomoka na ushindi lakini mara nyingi soka ni mchezo ambao huwa wa maajabu sana hususan klabu ambazo hazipewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri zinaposhushiwa hadhi hiyo hivyo bado mechi ni ngumu kwa wote.

Dakika ya 12 ya mchezo Luke Shaw alijifunga kwa kuugusa mpira uliokuwa umepigwa kuelekezwa kwenye lango lao wakati akijitahidi kuuokoa mpira huo. Kitu ambacho kilifanya mechi hiyo kuisha katika hali hiyo bila kupatikana kwa matokeo mengine na kuona kwamba timu hizo zilicheza kwa tahadhari sana.

Ushindi walioupata mbele ya PSG bado unawapa nguvu kwamba lolote linaweza kutokea kwenye mechi yao japo wao wenyewe wanaamini awamu hii haiwezi kuwa rahisi kama ilivyokuwa awali kwenye mechi yao na PSG hivyo wanahitaji kujipanga kwa nguvu zote kuona wanavyoweza kupata matokeo.

Historia ya Barcelona wakiwa nyumbani bado inaweza kuwa ni kitisho kikubwa mbele ya United kutokana na aina ya soka ambalo hucheza. Sio wepesi wa kuachia mechi wakiwa mbele ya mashabiki zao ndani ya viwanja hivyo. Pia, watarudi viwanjani wakiwa na tahadhari iliyowatokea ndugu zao PSG.

Bado meneja anawaamini washambuliaji wake, Lukaku, Martial, Jesse na Rashford ya kwamba yeyote kati yao ana uwezo wa kubadili matokeo uwanjani kitu ambacho bado anakiona ni nafasi ya kikosi chake kwani hawa wana uwezo wa kuleta kashikashi mbele ya safu ya ulinzi ya Barcelona.

Japo United walionesha uwezo kiasi chake kupambana lakini safu ya ulinzi ya Barcelona ilionekana kuwa huru sana kutokana na Lukaku kuwafanya walinzi hao wajiachie na wafanye kile wanachoona wao sahihi. Uchezaji wa Lukaku ulikuwa wa kiwango cha chini sana ukilinganisha na umuhimu wa mechi hiyo kitu kilichofanya atolewe na kumuacha Martial aingie.

Japo mwalimu wa kikosi hicho amemkingia kifua kwa kusema kwamba inawezekana alichoka na hata hivyo wanashukuru kwa makubwa aliyoyafanya mbele ya Barcelona kutokana na matumizi sahihi ya mwili wake kuwazuia Barcelona wasiondoke na mipira kwa urahisi inapovuka eneo la katikati la safu yao ya washambuliaji.

3 Komentara

    United mmepotea tayari

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habari nzuri.

    Jibu

Acha ujumbe