Beki kitasa wa klabu ya Manchester United raia wa Ivory Coast Eric Bailly ana mpango kutimkia klabu ya Olympique Marseille.
Klabu ya Marseille imekubaliana na United kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo wa msimu mzima huku kukiwa na nafasi ya kumnunua jumla kama tu klabu ya Olympique Marseille itafuzu michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.
Beki huyo amekua akisumbuliwa na majeruhi tangu kujiunga na klabu hiyo kitu kilichomfanya kua nje ya uwanja kwa muda mrefu na kukosa nafasi ya kudumu kikosi cha Man united. Bailly anaondoka ndani ya United kutokana na ufinyu wa nafasi ndani ya kikosi hicho ambapo kimesheheni mabeki wengi wa kati huku yeye akionekana sio kipaumbele cha mwalimu Eric Ten Hag.

bailly, Bailly Kutimkia Marseille kwa Mkopo., Meridianbet

klabu ya Marseille pia ilipata changamoto katika mbio za kumpata beki huyo kutoka klabu ya As Roma inayofundishwa na ya nchini Italia inayofundishwa na kocha zamani wa United Jose Mourinho. Marseille wamefanikiwa kushinda mbio hiyo ya kumuwania beki huyo kitasa kwani wameshafikia makubaliano  ya kumpata mchezaji huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa