Balaa Jingine kwa Ousmane Dembele!

Nyota wa Barcelona Ousmane Dembele amepata kikwazo kipya siku chache tuu baada ya kurejea.

Nyota huyu wa Ufaransa alitumia takribani miezi mitatu msimu huu nje ya dimba kwa sababu ya changamoto za majeraha aliyoyapata akiwa na Ufaransa kwenye Euro 2020.

Dembele amekuwa na changamoto kubwa ya majeraja kwa miaka minne akiwa na Barcelona, bila shaka alikuwa anatamani sana kurejea dimbani baada ya jeraha lake la hivi karibuni, ikiwa ni msimu wa tatu mrefu wa kukaa nje kwa sababu ya changamoto ya majeraha.

Ousmane Dembele

Amerejea baada ya kuwa nje kwa gemu 14, alionekana kuwa na moto zaidi akitokea benchi wakati Barcelona wakiwachapa Dynamo Kyiv kwenye Ligi ya Mabingwa Jumatano.

Kwa bahati mbaya staa huyu amepata jeraha jingine leo, hii inamaanisha kuwa staa huyu atashindwa kucheza mechi ya wikiendi dhidi ya Celta Vigo na bado haijawekwa wazi kuwa ni lini atarejea.

Hata hivyo, kuna matumaini kuwa huenda akarejea baada ya takribani wiki mbili, huenda akashiriki mechi dhidi ya Espanyol ya November 20.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe