Balaa la Deontay Wilder, Anaweza Kuua!

Bingwa wa ngumi za uzani wa juu Deontay Wilder alitamba kuwa anapenda mchezo wake kwa kuwa ni mchezo ambao unaweza ukaua mtu na ukalipwa kwa kufanya hivyo akidai akisisitiza kuwa sharia za mchezo huu zinaruhusu.

Bingwa huyu anataka kuendelea kujiwekea rekodi nzuri wakati akijiandaa kutetea taji lake la Ubingwa wa Dunia –WBC Jumamosi dhidi ya Dominic Breazeale. Pambano hili linakuwa la kwanza kwa bondia huyu toka alipochapana na Tyson Furry mwezi Disemba ambalo lilimaliza kwa droo.

Katika maandalizi yake bondia huyu amenukuliwa akitamba kuwa ndugu wa mpinzani wake waandae kabiza mazingira ya mazishi ya ndugu yao. Wilder alishawahi kunukuliwa akiyoa matamshi kama haya mwaka Machi 2018.

Wlder vs Breazeale
Wilder vs Breazeale | Unaweza kuweka utabiri wako hapa BET

Akizungumza na vyombo vya habarai Wilder anasema kuwa maisha ya mpinzani wake yapo kwenye mstari, kwakuwa wapo katika mchezo wa hatari “Huu ndiyo mchezo ambao unweza ukamuua mtu na ukalipwa kwa shughuli hiyo.” –Wilder

Deontay Wilder ambaye ana miaka 33, ana rekodi ya Knock Outs 39 kwenye mapambano yako 40 aliyopigana. Wilder anahitaji kuweka rekodi kwa kumchakaza mpinzani wake Breazeale ambaye ana rekodi ya kupoteza pambano moja tu katika mapambano yake 21, alipoteza pambano lake dhidi ya Anthony Joshua mwaka 2016.

Acha ujumbe