Bale na Ramsey, Mnatuambiaje -Tunabaki au Tuondoke?

Pengine unaweza kudhani ni majina tu yamebaki lakini uwezo wao uwanjani ni suala jingine. Gareth Bale na Aaron Ramsey, bado wanakitu cha kuuthibitishia ulimwengu wa soka.

Baada ya kufanya vizuri na Spurs na baadae kwenda Real Madrid, Bale alikua kwenye kiwango bora wakati ule. Alipata mafanikio mengi akiwa Bernabeu lakini mambo yanabadilika, majeruhi na kukaa benchi akiwa chini ya Zidane kuliathiri uwezo wake uwanjani.

Mwenda kwao hutunzwa, Bale alirejea Spurs kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja ambao unaisha Juni 30,2021. Pamoja na kwamba muda wake ndani ya Spurs unaelekea ukingoni, kuna uwezekano wa Daniel Levy kutumia kipengele cha kuongeza muda wa mkataba kwa mwaka mmoja zaidi. Ikumbukwe, mkataba wa Bale na Madrid umebakiza mwaka mmoja tu, sasa ni arudi Madrid au abaki Spurs.

Mambo yamebadilika tangu ajiunge na Spurs. Mourinho amefukuzwa kazi Spurs, klabu sasa hivi inahaha kupata kocha mpya. Kule Bernabeu, adui wake mkubwa – Zinedine Zidane naye ameachana na timu hiyo na sasa Carlo Ancelotti amerejea kwenye nafasi yake ya miaka kadhaa nyuma.

Kwa sasa, Bale yupo na timu ya Taifa ya Wales ambao anaonesha ubora wake uwanjani. Baada ya kumalizika kwa mashindano ya Euro 2020, nyota huyo atakuwa na maamuzi ya kufanya – anarudi Real Madrid chini ya Ancelotti au atabaki Spurs kama atapendezwa na muelekeo wa timu hiyo?

Kwa Aaron Ramsey, hali yake kwenye ngazi ya klabu ni kama ilivyo kwa Bale. Umuhimu wao unaonekana kwenye Timu ya Taifa ambapo ni mihimili mikubwa ya timu hiyo. Ramsey aliondoka Arsenal kama mchezaji huru na kujiunga Juventus (2019), maisha ndani ya Turin yamekuwa mazuri kwa mda mfupi na mabaya kwa muda mrefu.

Majeruhi yamekuwa kikwazo kikubwa kwa Ramsey kuonesha ubora wake. Ujio wa Maximiliano Allegri ni kipimo cha Ramsey kuonesha ubora wake ili kuweza kupata namba kwenye kikosi cha timu hiyo, ataweza?

Arsenal, West Ham United na Crystal Palace zinahusishwa na usajili wa Ramsey lakini kiungo huyu anaamini bado anauwezo wa kucheza kwenye klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa, hakika baada ya mashindano ya Euro 2020 tutajionea mengi.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe