Tukiwa tupo katika wiki za mwisho kabisa za msimu wa ligi wa 2018/19 huku ligi nyingi zikiwa tayari zineamua mabingwa wake kama vike Hispania, Italia na Ufaransa. Lakini upande wa Uingereza na Ujerumani kukiwa bado na ugumu kujua nani anaenda kunyanyua kombe kutokana na ushindani na tofauti ya alama iliyopo kati yao.
Upande wa tuzo za Ballon d’Or kuna majina mawili ambayo kwa hakika yametawala kwa kiwango kikubwa katika sayari hii kuchukua tuzo hiyo; baada ya wawili hao kuchukua tuzo hiyo mara tano kila mmoja kukiwa hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufikia hatua hiyo ya kunyanyua tuzo hiyo kwa uwiano huo.
Kwa mwaka huu tuzo hiyo imebeba majina ya wachezaji kutoka vilabu vya Manchester City, Barcelona, Juventus, PSG, na Liverpool ambao wameingia kushindania nafasi zao hizo muhimu za kupata heshima hiyo ambayo imetawaliwa na wawili hao japo wawili hao bado wamo kwenye majina hayo.
Kuna majina ambayo kwa hakika yana uwezekano mkubwa wa kuingia katika kinyang’anyiro cha kuchuana nafasi tano za juu kwenye tuzo hiyo bora kabisa. Hiyo ni kutokana na msaada mkubwa waliovipa vikosi vyao msimu huu wa ligi unaoelekea kuisha. Baadhi yao ni kama vile:
Lionel Messi na Gerard Pique (FC Barcelona), wawili hawa wana nafasi kubwa ya kuunda nafasi tano za juu za wale watakaogombania tuzo. Messi kwa nafasi yake amekuwa msaada mkubwa ndani ya klabu yake hususan katika kutwaa kombe la ligi msimu huu na hata kuipeleka mbele kwenye michuano mikubwa klabu hiyo wakishirikiana na Messi kwenye safu ya ulinzi ya klabu.
Virgil van Dijk (Liverpool), nguzo ya ulinzi katika kikosi cha Liverpool msimu huu kwa hakika ameleta muunganiko wa aina yake ndani ya kikosi cha Majogoo hao. Ana nafasi kubwa sana kuingia kwenye nafasi hiyo ya kufanya vizuri kwenye tuzo hiyo.
Cristiano Ronaldo (Juventus), kutoka Hispania hadi Italia bado heshima yake inaendelea kusalia pale pale. Amekuwa na msaada mkubwa sana ndani ya kikosi hicho katika michuano japo walitolewa hatua ya robo fainali lakini pia katika ligi yao amekuwa nguzo imara sana mbele ya kikosi hicho.
Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain), ameonesha mafanikio makubwa akiwa na umri mdogo bado. Pamoja na kuondolewa kwao na United kwenye michuano ya klabu bingwa lakini bado ana nafasi ya kufanya vizuri kutokana na ukomavu aliouonesha ndani ya ligi, michuano na hata wakati wa kombe la dunia ambayo alishiriki na kuvunja rekodi za aina mbalimbali ambazo ziliwahi kuwekwa na watangulizi wake walipokuwa katika umri kama wake.
Povel
Cr7 yake hiyo