Mshindi wa taji la Ballon d’Or kwa mwanasoka bora wa kiume na wa kike duniani sasa ataamuliwa kutokana na matokeo yake katika msimu mmoja badala ya kalenda ya mwaka mzima jinsi ambavyo imekuwa.
Katika mabadiliko hayo, France Football ambao ni waandaaji wa tuzo hiyo ya haiba kubwa wameamua pia kupunguza idadi ya waamuzi au majaji wanaohusika kutafuta mshindi.
Jopo la wanahabari 170 ambao wamekuwa wakihusika awali sasa litakuwa na wanahabari 100 pekee watakaotafuta mshindi wa wanasoka wa kiume huku waamuzi 50 pekee wakihusika katika kusaka mshindi wa kike.
Wanahabari hao wanatokea katika mataifa yanayoshikilia nafasi za juu kwenye orodha ya viwango bora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
“Hapo awali, kigezo tulichotumia ni matokeo ya wanasoka katika nusu mbili za kampeni za msimu mmoja. Washindi wapya sasa wa Ballon d’Or watapatikana kutegemea matokeo yao kila msimu,” akasema mhariri wa jarida la France Football, Pascal Ferre kwa kusisitiza kwamba mabadiliko hayo yanachochewa na haja ya kuondoa utata na kurahisisha zaidi mchakato wa kutafuta mshindi wa kila kitengo au kipengele.
Hatua ya Lionel Messi wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Argentina kutawazwa mshindi wa Ballon d’Or mnamo 2021 ilizua mjadala mkali huku mashabiki. Wachambuzi na wadau wengi wa soka wakihisi kwamba Robert Lewandowski mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland ndiye alistahili kutwaa taji hilo.
Messi aliweka rekodi ya kutwaa Ballon d’Or kwa mara ya saba licha ya Lewandowski aliyeambulia nafasi ya pili kufunga mabao 41 katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) na kusaidia Bayern kuzoa taji la Bundesliga kwa mara ya tisa mfululizo.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.