Ballon d’Or ya Baadaye!

Siyo jambo la kushangaa sana kwa wachezaji wa aina yake kuonekana wanahusishwa sana na kuja kutawala soka kwa miaka ijayo. Kutokana na uwezo wake wa pekee kwa hakika anaonekana kuja kusumbua sana kwenye soka kutokana na uwezo wake ambao amekuwa akiuonesha hata kwa mechi zake za hivi karibuni.

Amekuwa ni mchezaji wa kuvunja rekodi kubwa nyingi ambazo ziliwekwa na kufikiwa na watangulizi wake kwenye soka. Kuna baadhi ya rekodi zinaonekana kuwa ngumu kufikiwa lakini nyota huyo ameweza kuzifikia nyingi ya rekodi hizo na kuzivuka kabisa. Jambo hilo kwa hakika linamfanya aonekane kuja kutawala soka mbeleni.

Ni mchezaji mwenye umri mdogo sana kuweza kufunga magoli kumi kwenye ngazi ya klabu bingwa; aliweza kujitangaza katika ulimwengu wa soka baada ya kufanikiwa kufunga idadi hiyo ya magoli akiwa na Monaco kwenye msimu wa 2016/17. Goli lake la kwanza lilikuwa dhidi ya Manchester City akiwa pia kwa upande mwingine aliandika historia hiyo akiweza kulingana na nyota mwenzie wa taifa hilo Karim Benzema. Aliendelea kufanya ivo pia kwa klabu nyingine kama Borussia Dortmund na Juventus.

Zaidi ya hayo, Mbappe aliweza kufunga goli lake la kumi akiwa na PSG katika mechi ambayo waliweza kupoteza kwa kipigo cha 3-1 mbele ya miamba hao wa soka wa Ujerumani. Kwa wakati wote huo alikuwa na umri wa miaka 18 pekee huku akiandika rekodi hiyo. Kwa maana hiyo aliweza kuvunja rekodi ya Benzema na ile ya Messu ambaye aliweza kuiweka akiwa na miaka 21.

Mchezaji mwenye umri mdogo kucheza mechi 30 za timu ya taifa, baadhi ya wakongwe wa taifa hilo waliweza kucheza ndani ya taifa hilo mechi nyingi sana, lakini wengi wao hawakuweza kufikia rekodi hiyo wakiwa na umri wa Mbappe. Baadhi ya nyota kama Zinedine Zidane, Michel Platini, Thierry Henry ba wengineo waneweza kulichezea taifa hilo mechi nyingi sana kwa mafanikio lakini bado Mbappe anaendelea kushikilia zaidi rekodi kubwa mbele yao.

Mchezaji mwenye umri mdogo kuweza kufunga magoli 30 ndani ya msimu, historia hiyo ya kipekee aliyoweza kuiweka inamfanya nyota huyo aweze kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri wa chini sana kuweza kufikia idadi hiyo ya magoli kwa msimu mmoja ndani ya ligi hiyo ya Ufaransa. Kiwango hicho alikifikia baada ya kufunga magoli matatu ndani ya mechi moja akiwa na Monaco. Aliweza kuvunja rekodi iliyowekwa na Jean-Pierre Papin miaka ya 1989-90.

Pia, rekodi yake nyingine ni ile ya kufunga magoli  kwenye kombe la dunia; Mbappe aliweza kufunga goli katika fainali za kombe la dunia na kufanikiwa kuandika historia ndani ya michuano hiyo huku akiweza kuifikia rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Pele kwa kipindi chote tangu mwaka 1958. Kwa takwimu hizo nyota huyo anakuja kwenye kizazi cha kuanza kutwaa tuzo mbalimbali kutokana na kiwango chake kikubwa alichonacho na historia yake.

Acha ujumbe