Balotelli Kulamba Mara 4 ya Mshahara!

Ripoti zinamtaja nyota Mario Balotelli kuwa anaweza kulipwa mara 4 zaidi ya mshahara ambao anatakiwa kulipwa.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali staa huyu aliamua kujiunga na klabu yake ya nyumbani na kukubali kupungua kwa mshahara wake ukilinganisha na pesa aliyokuwa akilipwa akiwa OGC Nice na Olympique Marseille.

Pia vyanzo vingine vimetaja kuwa kuna taarifa zilizojificha kuhusu hali ya mkataba wa staa huyu na klabu ya Brescia.

Mshahara wa sasa kwa mkataba ambao ameusaini staa huyu ni paundi milioni 1 kwa mwaka. Mkataba huu unatajwa kuwa umehusisha bonasi ambazo zinaweza kufikisha mara 4 ya mshahara wake kama atafanikiwa kufunga magoli mengi.

Kama staa huyu akifanikiwa kufunga magoli angalau 15, kwa msimu kwenye Serie A basi atapata malipo ya paundi milioni 4 kwa mwaka, mara 4 ya mshahara wake.

Lengo ni linatajwa kuwa ni klabu ya Brescia kujihakikishia usalama na kutoboa zaidi kwenye Serie A. Mpaka sasa amefunga goli 1 kwenye mechi 2 alizocheza.

Acha ujumbe