Licha ya kuwa katika hali ngumu kiuchumi, Barca wanamalengo makubwa ya kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao.

Idara ya kiungo na ushambuliaji ni maeneo yanayoangaliwa kwa umakini mkubwa na Xavi Hernandez kuelekea msimu ujao. Akiwa amekabidhiwa timu katikati ya msimu huu, kocha huyu anaendelea kukiangalia kwa ukaribu kikosi cha Barca kuelekea mwishoni mwa msimu.

Erling Haaland na Robert Lewandowski ni miongoni mwa washambuliaji nyota wanaotajwa kule Camp Nou. Lakini, linapokuja suala la pesa, FC Barcelona hawana ubavu huo kwa sasa. Haaland anatajwa kule Man City huku Lewandowski huenda akasalia Bayern Munich.

Barca

Kwenye orodha ya washambualiaji wanaotizamwa na Barcelona kuna Romelu Lukaku. Amerejea Chelsea msimu huu akitokea Inter Milan lakini, maisha yamekuwa magumu kwa Lukaku ndani ya Stamford Bridge na, dalili zinaonesha huenda akaondoka baada ya msimu huu kuisha.

Hii ni fursa kwa Barca lakini, Chelsea hajalipa pesa waliyokubaliana na Inter Milan kwenye usajili wa Lukaku kwenda The Blues. Takribani £77M bado hazijalipwa na hii inaweza kufanya usajili huu kuwa mgumu kwa pande zote zinazohusika.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa