Barca Walidunda Kumsajili Kane

Klabu ya Tottenham inaripotiwa kuwa ilikataa ofa ya Barcelona ya kumnunua Harry Kane msimu wa joto uliopita.

Barcelona wamekuwa sokoni wakisaka mshambuliaji mpya wakati Luis Suarez akionekana yuko ukingoni mwa mda wake katika soka.

Kwa mujibu wa chapisho la Mundo Deportivo, Barcelona wamekuwa wakipanga kwa mda mrefu kumpata mrithi wa Suarez na wameona Kane ni mbadala anayefaa kurithi nafasi hiyo.

Klabu ya Tottenham inaripotiwa kuwa ilikataa ofa ya Barcelona ya kumnunua Harry Kane msimu wa joto uliopita.
Harry Kane

Barcelona wanasema walijaribu kumsajili Kane lakini walitolewa nje na ada kubwa ya usajili iliyotajwa na mwenyekiti Daniel Levy.

Kwa sasa inadhaniwa kuwa Barcelona hawatatarajia kuejea kuwabembeleza Spurs katika manunuzi yao ya msimu ujao wa uhamisho. Wanatarajiwa kuwa watatumia mteremko wa janga la corona ili kumnasa straika kutoka Serie A.

Kutoka Italia, mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez ndiye yupo kwenye orodha ya wanaowindwa zaidi na Barcelona.

Wakati huo, Kane alishaweka wazi kuwa atalazimika kusepa Spurs ikiwa vijana hao wa Mourinho watashindwa kufanya mapinduzi na kupata mafanikio ya haraka ikiwa ni pamoja na kushinda mataji muhimu ikiwa ni pamoja na Ubingwa wa Ulaya.

40 Komentara

    Duuh kwanini walikataa jamani

    Jibu

    Ken ni mshambuliaji ambaye huwa nampenda Sana hasa akiwa ktk safu yake ya ushambuliaji anajua kucheza na mpira

    Jibu

    tottenham wanatikisa kiberiti tu, maana hawajawekewa dau la kutosha, barca wakipandisha dau la kutosha wenyewe wataachia

    Jibu

    Tatizo la wachezaji wa kiingereza wanawapamba Sana na kuwauza pesa nyingi ,Naukiangalia baca hawana pesa kwa sasa

    Jibu

    Kwann wamekataa kumsajiri Kane kiungo mzuri uyo

    Jibu

    Barcelona mkipambana mtampata tu kane #meeidianbettz

    Jibu

    Kane yuko vizuri kumbe mpaka dau lake ni kubwa hivyo.

    Jibu

    Inabidi waongeze dau maana Ni mchezaji mzuri sn

    Jibu

    Mbona yupo vizuri

    Jibu

    Club ya Simba wanamtaka sana huyu jamaa#Meridianbettz

    Jibu

    Kane ni mchezaji mzur alistahili kwenda Barca ila dau ndio limemwangusha

    Jibu

    Kane fundii barcelona waongeze dau..

    Jibu

    Duh hatar basi #meridianbet

    Jibu

    Tanga nao weingilia Kati kwenye usajili wake

    Jibu

    Barcelona wajitahidi kupambana wampate kane

    Jibu

    Du meridian mko juu

    Jibu

    asanteni kwa habari za uhakika

    Jibu

    Barcelona wangempoteza kiwango Kane

    Jibu

    Kane jembe

    Jibu

    Why mbona kane mchezaji mzuri sana jamn

    Jibu

    Kene yuko vizuri sana na amekuwa bora zaidi katika timu ya Tottenham

    Jibu

    Awakuwa nania ya kumsajili #meridianbettz

    Jibu

    gud newz

    Jibu

    Kwa safu ya Barcelona ya ushambulizi angesumbua sana

    Jibu

    Yupo vizur

    Jibu

    Good news 👍@# meridianBetTZ

    Jibu

    thnks meridian bet tz

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    thnks meridian kwa information

    Jibu

    Daaah

    Jibu

    Hyu dgo ni fundi sana

    Jibu

    Da!

    Jibu

    Asnte meridian kwa habari

    Jibu

    Huyu anafaa kucheza EPL tu ligi zingine hazimuwezi abaki zake spurs

    Jibu

    Wangekua moto sana kama wangempata kane

    Jibu

    Kane hanajua sana..!

    Jibu

    kane yupo vzr sana#meridianbettz

    Jibu

    Kane ni mzuri sana ila sio wa aina ya uchezaji wa barca

    Jibu

    Kane ni mshambuaji mzuri.ila kwa waingereza wagumu kutoka nchi .

    Jibu

    Habari njema na #meridianbet

    Jibu

Acha ujumbe