Mlipuko wa virusi vya COVID19 umetikisa uchumi wa kila sekta. Kwenye sekta ya michezo, klabu mbalimbali ikiwemo Barcelona zilitikiswa na virusi hivyo.

Kufuatia kuporomoka kwa uchumi, klabu zilihitaji kuchukua hatua za tahadhari ili kunusuru ajira za wachezaji pamoja na wafanyakazi wengine kwenye vilabu vyao.

Arsenal ni miongoni mwa timu ambazo zilipunguza idadi kubwa ya wafanyakazi pamoja na kupunguza mishahara ya wachezaji. Barcelona wamefuata nyayo katika hilo na watafanikiwa kuokoa kiasi cha Euro milioni 122 mwishoni mwa msimu huu.

Barca wanafikia hatua hii baada ya wachezaji wa timu hiyo kukubali kupunguziwa mishahara ili klabu hiyo iweze kuwalipa mishahara wafanyakazi wengine ambao sio wachezaji.

Huu ni muendelezo wa ari ya kujitolea kwa wachezaji wa Barca baada ya mwezi Machi kukubali kupunguziwa mishahara yao kwa 70%. Barca waliripoti kupata hasara ya pauni milioni 87 huku deni la timu hiyo likiongezeka mara mbili na kufikia pauni milioni 438.

Taarifa rasmi kutoka Barca inasema “hii ni hatua kubwa katika kubadilisha hali ya kiuchumi kwa sasa”.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa