Klabu ya Barcelona bado inamatumaini ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Chelsea Marcos Alonso kabla ya dirisha la usajiri kufungwa baada ya kufanikisha kuwasijiri wachezaji kadhaa mpaka sasa.
Baada ya klabu ya chelsea kufanikisha usajiri wa Marc Cucurella kwa kiasi cha £62million kuna toa mwanya kwa Alonso kuweza kuoneshewa mlango wa kutokea huku Barcelona likiwa ndio chaguo pekee baada ya kuonesha nia ya kuhitaji huduma ya mlinzi huyo.

Marcos Alonso shauku yake kwa sasa ni kutaka kurejea nyumbani nchini Hispania ili aweze kuwa karibu na familia yake. Alonso ametumia miaka sita kwenye viunga vya Stamford Bridge huenda dirisha hili likiwa ndio mwisho wa maisha yake jijini London.
Mkataba wa Alonso na Chelsea unatamatika mwaka 2023, ikiwa barcelona watahitaji huduma yake basi itabidi walipe gharama kidogo ili waweze kuvunja mkataba wake.

