Barcelona Kumsajili Martinez Kama Mbadala wa Suarez

Klabu ya Barcelona imeripotiwa kuwania saini ya nyota wa Inter Milan Lautaro Martinez kama mbadala wa Luis Suarez katika dirisha hili la usajili.

Kocha mpya wa klabu ya Barcelona, Ronald amesema kuwa Suarez hayupo katika mipango yake ya msimu ujao hivyo kuwataka Barcelona waongee na mchezaji huyo kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na nyota huyo.

Martinez Kama Mbadala wa Suarez
Luis Suarez hayupo katika mipango ya Ronald Koeman

Koeman alietambulishwa kama kocha wa wababe hao wa Catalunya mwezi huu kuchukua nafasi ya Quique Setien aliyefurushwa baada ya kipigo cha 8-0 kutoka kwa Bayern Munich katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, amepanga kukifanyia marekebisho makubwa kikosi hicho

Hali mbaya ya kiuchumi na migogoro katika uongozi wa klabu hiyo unafanya hatima ya wachezaji wengi wa timu hiyo kuwa katika hatihati, hili la Suarez linakuja ikiwa hatima ya Lionel Messi na nyota wengine wa kikosi cha kwanza ndani ya klabu hiyo bado haijajulikana.

Licha ya kuambiwa na Koeman kuwa hayupo katika mipango yake ya msimu ujao, Luis Suarez ameripotiwa kuwa anapendelea kuendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho lakini hilo litategemea maamuzi ya viongozi wa juu wa klabu.

Luis Suarez aliejiunga na Barcelona mwaka 2014 amekua na mafanikio makubwa klabuni hapo. Suarez amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa pili kwa muda wote aliodumu katika kikosi hicho nyuma ya Lionel Messi. Msimu uliopita alifanikiwa kuifungia Barcelona jumla ya magoli 24 katika mashindano yote (La Liga, Mechi za Kirafiki na Ligi ya Mabingwa Ulaya).


 

Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

38 Komentara

    martinez si haba naye yupo vizuri katika soka tunataka kuona ushirikiano wake katika timu

    Jibu

    dah kumbe kweli Suarez anaondoka Barcelona😭

    Jibu

    Koeman kweli anataka kuweka mabadiliko ndani ya club ya barca.

    Jibu

    Daah sasa itakuajee

    Jibu

    Duuh hii habari mbaya kwa wapenzi wa barcelona

    Jibu

    Habar njema kwa mashabik wa barcelona Kama dili hlo litakamilik replacement sahh ila suarez hawamtendeh haki Kama watamwacha kuondok hv hv bila hata party ya kumuaga legendary hyo

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki

    Jibu

    Ni habar njema na mchakato mzur wa koeman kutaka kumsajil Lautaro Martinez
    ambaye n kijana kabisa mbadala wa Luis suarez ambaye umri umeshaeenda sana 👍 nimeupenda huo usajil

    Jibu

    Ni habari mzuri kwa mashabiki

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Kutokana na hali ya uchumi tuu ndio itasababisha Barcelona wasiweze kukaa na wachezaji wote wawili yaani Suarez na Martinez ila ingekuwa jambo zuri kama wote wangekuwepo Barca ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa makombe

    Jibu

    iko poa sana

    Jibu

    Karibu martinezi.

    Jibu

    For me ni chaguo sahihi

    Jibu

    Maamuzi sahihi!!!

    Jibu

    Matinez duh ni noma

    Jibu

    Sio mbaya ila kocha anatakiwa akisuke kikosi chake ipasavyo maana Barcelona ya Sasa mauza uza

    Jibu

    Nadhani mwalimu anajua kwamba mbadala wake ndio huu.

    Jibu

    Huyo ni mchezaji mzuri anaweza kua mbadala wa Suarez.

    Jibu

    Suarez atafute klabu nyingine ya kuitumikia tu amalizie miaka yake

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wa Barcelona

    Jibu

    Koemon kweli anataka kuleta mabadiliko ndan ya barca#Meridianbettz

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wa barcelona

    Jibu

    Daah Sasa itakuajea

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Uamuzi mzuri

    Jibu

    Hii balaa

    Jibu

    Koemani anataka kuleta mabadiliko
    @meridianbettz

    Jibu

    iko poa

    Jibu

    Barcelonaa duuh itakuaje

    Jibu

    Uamuzi huo ni fresh

    Jibu

    Chaguo zuri

    Jibu

    Duh maisha yanabadirika kwa kasi kubwa kutoka kwenye utatu maridhawa Messi na Naymar hadi kuonyeshwa mlango wa kutokea! Bado suarez ana uwezo mkubwa wa kufunga endapo atacheza timu sahihi#meridianbettz

    Jibu

    Suarez umri ushamtupa mkono.

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Duu Sasa itakuwaje Barcelona ndio washaamua huwamuzi wao Suarez ndoanandoka jembee daa

    Jibu

    Habar njema kwa mashabik wa barcelona Kama dili hlo litakamilik replacement sahh ila suarez hawamtendeh haki Kama watamwacha kuondok hv hv bila hata party ya kumuaga legendary hyo

    Jibu

    Wako Vizuri sana

    Jibu

Acha ujumbe