Barcelona wamewasilisha offer yao kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Poland anayekipiga kwenye klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani lakini mpaka hawajapatiwa majibu yoyote.

Lewandowski aliweka wazi kuwa anahitaji kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu, na yuko tayari kujiunga na klabu ya Barcelona, japo maendeleo ya usajiri wake yamepungua kasi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Lewandowski mwezi unaokuja anatimiza miaka 34, na kwenye msimu uliyoisha amefanikiwa kuifungia klabu ya Bayern Munich magoli 50, kwenye mashindano yote na kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi kwenye ligi kubwa tano barani Ulaya.

Raisi wa klabu ya Barcelona Joan Laporta wakati akiwatambulisha wachezaji wapya waliosajiriwa na klabu hiyo ambao ni  Franck Kessie na Andreas Christensen, kwenye dimba la Camp Nuo, alinukuliwa akisema.

“Tumeshapeleka offer kwa Lewandowski, na tunasubiri majibu kutoka Bayern Munich. Nataka nimshukuru mchezaji kwa ishara yake ya kutaka kuja. Bayern Munich inapaswa kuitathmini offer yetu, na sisis tunasubiri majibu.”


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa