Klabu za Barcelona, Liverpool na Chelsea wanaripotiwa kumtaka kiungo wa kati wa Benfica Enzo Fernandez mwenye umri wa miaka 21.
Fernandez aliwasili Benfica akitokea River Plate miezi minne iliyopita mwezi Juni kwa ada ya Euro milioni 10, na mara moja akatwaa Ligi Kuu ya nchini humo, huku ligi ikimtaja kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti.
Tangu wakati huo ameisaidia Benfica kufikia rekodi ya kutopoteza michezo waliyocheza ambapo wameshinda michezo 8, wamepata sare 1 na kwenye Ligi ya Mabingwa wameshinda michezo miwili na sare mbili.
Mchezaji huyo amecheza kila mchezo, na kiwango alichokionyesha dhidi ya Psg kwenye sare mbili mfululizo kimewavutia vilabu vingi vikiwemo Barcelona Chelsea pamoja na Liverpool vikihitaji huduma yake.
Kulingana na ripoti kutoka Sport, Barcelona walipata nafasi ya kumsajili Fernandez kwa €10m lakini wakasitisha usajili huo na kuruhusu Benfica kuingia kwa haraka, na sasa inatajwa kuwa thamani yake imepanda hadi kufikia € 50m..
Idadi hiyo inaweza kuendelea kuongezeka pia, huku akiwa amecheza mechi yake ya kwanza ya Kimataifa kwa Argentina mnamo Septemba, Fernandez anaweza kuwa na jukumu kubwa katika kampeni ya Kombe la Dunia ya nchi yake wanapoingia kwenye dimba kwa mfululizo wa mechi 35 bila kupoteza.
Ripoti hiyo inadai Barcelona itakabiliwa na upinzani kutoka kwa wababe wa Ligi Kuu ya Uingereza, Liverpool na Chelsea, ingawa hakuna dalili kwamba Benfica watakuwa tayari kumwachia Fernandez kwa miezi sita katika mkataba wa miaka mitano, klabu ambayo italeta ofa kubwa zaidi wanaamini kuwa hawawezi kukataliwa.