Waswahili husema ‘kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho’. Msemo huu unaendana na makubaliano ya Barcelona na Liverpool ya mwaka 2018.

Moja ya usajili mkubwa uliofanyika mwaka 2018, ulikuwa ni wa Philipe Coutinho aliyetokea Liverpool na kujiunga na Barcelona kwa dau la pauni milioni 145.

Liverpool walitengeneza pesa ndefu iliyofanikisha usajili wa Virgil van Dijk, Alisson Becker na Fabinho. Hawa ni wachezaji walioisadia Liverpool kutwaa ubingwa wa EPL msimu uliopita pamoja na kubeba kombe la Ligi ya Mabingwa – UEFA.

Mkurugenzi wa michezo wa Liverpool – Michael Edwards aliamua kuwakingia kifua Barca kwa kuweka kipengele kwenye mkataba wa Coutinho ambacho kingewahitaji Barca kuongeza pauni milioni 89 kwenye dau lolote ambalo wangetoa kumsajili mchezaji yeyote wa Liverpool kabla ya 2020 kuisha.

Barcelona, Barcelona Mbioni Kuwavamia Liverpool, Meridianbet
Philipe Coutinho Baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Barcelona akitokea Liverpool 2018.

Kwa hesabu za haraka haraka, unaweza kuunganisha matukio kwamba ni kwasababu gani Sadio Mane na Girginio Wijnaldum hawakusajiliwa na Barca japo timu hiyo ilisemekana inahitaji saini za wachezaji hao? Jibu rahisi, walikuwa wanakwepa kipengele cha kulipa pauni milioni 89 zaidi ya dau watakalotoa kuwasajili wachezaji hao.

Sasa 2020 inaelekea ukingoni na sasa ni rasmi, Barca wanaweza kuja kuivamia Liverpool na kuwasajili wachezaji wanaowataka kutoka kwenye kikosi hicho kwa bei halisi zaidi.

Soka ni biashara na katika hili, endapo Barca watafanikiwa kusajili mchezaji yeyote wa Liverpool mwezi Januari au hata dirisha kubwa la usajili mwishoni mwa msimu huu, basi watakuwa wamelamba karata dume na wameokoa pesa ndefu ambayo pengine ingewapa faida kubwa Liverpool kama usajili ungefanyika kipindi ambacho kipengele hicho bado kinatumika kwenye mkataba wa usajili wa Coutinho.

Je, Barcelona watafanikiwa kuwang’oa Sadio Mane na Wijnaldum kwenye kikosi cha Klopp?


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

  1. Vipengele hivi vya mikataba vimekuwa vikinufaisha sana baadhi ya timu, Chelsea imefaidika mno kumuuza Eden Hazard Real Madrid hususani baada ya kuchukua ubingwa wa La liga

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa