Klabu ya Barcelona imepanga kuwaomba wachezaji wa kikosi cha kwanza Jordi Alba, Gerard Pique na Sergio Busquets kupunguza mishahara ili kuweza kuokoa kiasi cha €100 million ili kupata nafasi ya kuweza kuobgeza wigo wa kuweza kusajiri majina makubwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi.
Uongozi wa klabu ya Barcelona unafanya kila liwezekano ambalo lipo ndani uwezo wao ili kupunguza gharama za mishara kwa msimu 2022-23 ili kuweza kufanya maingizo mapya.
Mpaka sasa tayari washaingia makubaliano na Kampuni ya CVC kuhusu haki ya matangazo television ambao unathamani ya €300 million, huku pia wakiwa wameingia makubaliano na kampuni nyingine ambao unathamani €350 million, licha ya pesa hizo zote kuingizwa kwenye mapato ya kumbukumbu za hesabu za mwaka.
Kwa sasa, klabu ya Barcelona iko sawa kwenye upande wa kifedha lakini bado wana ukomo wa kufanya matumizi, hivyo kwa hivi karibuni wamekuja na njia nyingine tena ya kuongeza wigo wa matumizi kwa kupunguza mishahara na bonusi za wachezaji wake wake watatu wa kikosi cha kwanza ili kuongeza kiasi cha €100 million kwenye matumizi.
Klabu imepanga kufanya nao mazungumzo ya kuwaomba kupunguza kiasi cha mshahara na bonusi kwa kila mmoja baada ya msimu huu kuisha.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.