Roma Waikataa Spurs

Dirisha la usajili bado linazidi kushuhudia klabu mbalimbali zikifanya maingizo kwenye vikosi vyao ili kujijenga kiushindani kwa ajili ya msimu ujao. Kama ilivyokuwa msimu huu, safari haikuwa nyepesi kwa baadhi ya timu kubwa mara baada ya kupata ushindani ambao wao wenyewe hawakuamini kwa haraka kama ingetokea.

Aston Villa wavutiwa na Tuanzebe, baada ya kucheza ndani ya klabu hiyo kwa mkopo msimu huu na kuifanikishia makubwa klabu hiyo hadi kupanda nafasi ya kucheza ligi wameona thamani yake na wanaonekana kutaka kumsajili nyota huyo kwa mkataba wa kudumu ili waweze kufanya naye kazi msimu ujao. Wanachokisubiri wao ni kama klabu inayommiliki nyota huyo itakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo kwa dau lililowekwa mezani ambalo ni £8m.

Barcelona na Valencia wataka biashara ya kubadilishana, matajiri hao wa soka Hispania wanaona kwamba kunaweza kukawa na unufaikaji kwenye biashara hiyo kwa sababu mlinda mlango wa Cillessen na yule wa Valencia, Neto thamani zao zinalingana na wao wanalikuwa na nia ya kufanya biashara. Kwa maamuzi wameamua kuwasogelea majirani zao Valencia ili waweze kukamilisha dili hilo. Thamani ya walinda mlango hao ni £30m, kinachoangaliwa ni kama wataweza kukaa mezani na kuliweka sawa.

Costa yupo Yupo, kulikuwa na taarifa zilizokuwa zimeanza kusambaa kwamba majirani wa United walikuwa mbioni kutaka kusajili mlinzi huyo lakini wamekanusha kwamba kwa sasa nafasi yao sio kuangalia tena mlinzi bali wanachoangalia ni nafasi nyingine. Wameweka wazi kwamba hawana mahitaji yoyote na nyota huyo hivyo majirani zao waendelee na mipango yao. Nyota huyo amekuwa na kiwango cha pekee sana kiasi cha kuwavuta wengi kutaka kumnasa.

Douglas Costa hajafikiria kuondoka Italia, nyota na raia wa Brazil ambaye anasifika kwa kuwa na kasi ya ajabu ndani ya soka anasema bado hajafikiri kabisa suala la kuondoka klabuni hapo pamoja na kwamba klabu ya PSG inaonesha kuwa na nia ya kumhitaji ili aweze kukaa katika kikosi chao. Mbali na fununu hizo anasema anaona atakua kisoka zaidi akiwa na Juventus na furaha yake kwa sasa ni kufanya kazi na uongozi mpya uliotua klabuni hapo mapema wiki hili hivyo ataendelea kusalia ndani ya jiji hilo.

Roma watema ofa ya Spurs, klabu hiyo ya nchini Uingereza walikuwa wanamfukuzia nyota huyo wa Roma na kiwango walichokitenga kwa ajili ya Nicolo Zaniolo kimezuiwa na matajiri wa kikosi hicho. Hawawezi kufanya biashara kwa fungu hilo la £63m kwa sasa. Kinachotakiwa ni wajipange upya kama wanataka kutuma ofa hiyo na kama kweli wanamhitaji nyota huyo ili aweze kuwapa huduma.

4 Komentara

    Hasanteni kwa habar nzuri#meridian

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    habari nzuri

    Jibu

    Habar nzuri

    Jibu

Acha ujumbe