Taarifa zinasema kuwa Barcelona bado wanendelea na mazungumzo ya mkataba mpya na nyota wake Ousmane Dembélé, lakini suala la uvumilivu linaonekana linaelekea ukingoni kwa klabu hiyo.
Staa huyu amekuwa nje ya uwanja toka alipopata jeraha kwenye Euro 2020 na kufanyiwa upasuaji.
Uvumi ulieleza kuwa klabu ya Barcelona ilikuwa na mpango wa kumuuza staa huyu kuelekea msimu huu, akiwa amesalia na mwaka mmoja tuu kwenye mkataba wake na kuwa meshindwa kufanya vyema sana toka alipowasili kwa €100m mwaka 2017.

Hata hivyo, changamoto ya majeraha ilionekwana kukwamisha mipango ya uhamisho ya staa huyu. Ousmane Dembélé kwa sasa anajiandaa kurejea dimbani, kukiwa na uwezekano wa yeye kucheza kwenye mechi dhidi ya Alves wikiendi.
Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Barcelona wanajaribu kufanya jitihada za kumshawishi staa huyu kusaini makubaliano ya mapya kwa kuwa wanahofia kumpoteza bure msimu ujao wa joto.
Kwa sasa mazungumzo juu ya mkataba mpya bado yanaendelea, wakati Ousmane Dembélé akitajwa kuwa yeye anataka kusalia klabuni hapo, Barcelona hawatarajii kumsubiri kwa mda mrefu kabla ya kuamua kufanya maamuzi magumu.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.
CHEZA HAPA