Raisi wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amevurugana na wachezaji wake akiwemo kapteni wa klabu hiyo kwa kutamka hadharani kuwa wachezaji wa klabu hiyo wanapaswa kupunguza mishahara yao ili kuweza kuinusuru klabu hiyo.

Mapema wiki hii, Sergio Busquets alimjibu raisi wa klabu Barcelona, Joan Laporta akisema kwamba ingekuwa bora kusikia taarifa hizo kutoka ndani ya klabu kuliko kusikia maneno hayo kutoka kwa vyombo vya vya habari.

Barcelona

“Kupunguza mshahara?, Ningependa klabu iniambie mimi mwenyewe, sio kusikia kupitia njia nyingine. Mara zote nimekuwa na nia ya kuisaidia klabu. Hawajaleta ombi lolote kwetu, kutoa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari sio njia sahihi. Mara zote tumekuwa na nia ya kuwasaidia.” Alisema Sergio Busquets

Mpaka sasa kulingana na taarifa kutoka kwenye viunga vya Catalunya, kuna taarifa inasema kuwa rais wa Barcelona, Laporta amemuomba radhi yeye binafsi Sergio Busquets na kumwambia kuwa apuuze taarifa za vyombo vya habari, na kumhakikishia kuwa mkataba wake hautaguswa na hakuna atakachopunguziwa kwenye mshahara wake.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa