Barcelona Waachana na Antonio Rudiger

Klabu ya Barcelona imerpotiwa kuachana na mpango wake wa kuhitaji huduma ya mlinzi wa klabu ya Chelsea ambaye mkataba wake unakwenda mwishoni kutokana na mlinzi wao Ronald Araujo kuonesha nia ya kukubali kusaini mkataba mpya.

Ronald Araujo anatarajiwa kusaini mkataba wa muda mrefu na klabu ya Barcelona  baada ya mazungumzo yao kufanikiwa kati ya pande zote mbili na kuweka mambo sawa mapema wiki hii.

Viongozi wa Barcelona walifanya kikao na wakala wa Rudiger wiki iliyopita ambapo ilipelekea kuzunguka kwa tetesi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani yuko njiani kuelekea kwenye viunga vya Camp Nou kwenye dirisha la majira ya kiangazi.

Barcelona walikuwa wanafikilia kuhusu uajari wake, Lakini mara zote kipaumbele chao ilikuwa ni kumuongezea mkataba mlinzi wao Araujo. Sababu nyingine iliyopelekea kusitisha uhamisho wa Rudiger ni swala la mshahara wake kuwa mkubwa na ada kubwa ya uhamisho wake.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe