Nyota wa Barcelona Sergi Roberto amepima virusi vya corona na kupatikana na maambukizi, klabu imetangaza.

Roberto, ambaye aliumia paja kwenye mechi dhidi ya Atletico Madrid mwezi uliopita, tayari alitakiwa kusalia nje ya uwanja hadi Januari kutokana na changamoto ya jeraha.

Barca iliripoti Jumatano kwamba Roberto “ana afya njema na anatengwa nyumbani”.

Barcelona Sergi Roberto

Taarifa ya klabu imeongeza zaidi kuwa tayari imewafahamisha maafisha wa afya na vitengo vyote vunavyohusika klabuni hapo, huku watu wote wa karibu wanaotajwa kuwa na mawasiliano, na huenda walikutana na staa huyu hivi karibuni wakifuatiliwa kwa ukaribu kupata vipimo.

Beki huyu wa kulia Roberto alikuwa amepata nafasi ya kuanza katika michezo saba kati ya nane ya Barcelona kabla ya kupata jeraha lake, licha ya kusainiwa kwa Sergino Dest kutoka Ajax.

Dest alimtangulia Roberto kwenye Clasico ya Oktoba, ambayo Real Madrid ilishinda 3-1.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania – pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo – amefunga mara moja kwenye mechi ya LaLiga msimu huu, akitoa usaidizi wa magoli mara 2 katika nafasi 10 alizotengeneza.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Barcelona, Barcelona Watangaza Sergi Roberto Kuambukizwa Corona, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

20 MAONI

  1. Beki huyu wa kulia Roberto alikuwa amepata nafasi ya kuanza katika michezo saba kati ya nane ya Barcelona kabla ya kupata jeraha lake, licha ya kusainiwa kwa Sergino Dest kutoka Ajax.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa