Timu ya Barcelona imeingia kwenye radar za kutaka kunyakua saini ya mchezaji wa Chelsea Jorginho kwa mabadilishano na kiungo wao Miralem Pjanic endapo Chelsea watahitaji huduma ya mchezaji huyo.

Jorginho amekuwa na kipindi kizuri katika timu ya Chelsea lakini kocha wa timu hiyo Thomas Tuchel ana mipango mikubwa msimu ujao ikiwemo kumsajili Miralem Pjanic ili kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji.

Barcelona wanategemea kuendelea kubaki na Pjanic kutokana na uwezekano wa Wijnaldium kusadikika ataondoka mwisho wa msimu huu. Na kigezo pekee cha kumuachia mchezaji huyo ni kubadilishana na Jorginho, ambaye amekuwa akifanya vyema sana toka ujio wa Tuchel pale darajani.

Tuchel amekuwa mpenzi mkubwa wa Pjanic toka alivyokuwa PSG na anaamini anaweza kuwa ingizo bora na muhimu sana kwenye timu ya Chelsea ambayo ina malengo makubwa sana msimu ujao.

Pjanic hajawa na msimu mzuri sana pale Camp Nou msimu huu, huku akiwa amecheza michezo 28 na hajafanikiwa kufunga goli wala kutoa pasi ya magoli. Pia, hajacheza mchezo wowote wa La Liga toka mwezi Februari mwaka huu.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Jorginho, Jorginho Kuwa Mbadala Wa Pjanic Barcelona, Meridianbet

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa