Nyota wa Benfica Darwin Nunez atasalia kwa miamba wa Ureno hadi angalau 2022 wakati akiwa anahusishwa na klabu ya Barcelona, ​​hii ni kwa mujibu wa wakala wake Edgardo Lasalvia.

Nunez amekuwa mchezaji wa gharama sana kusajiliwa na Benfica –alipowasili kutoka Almeria kwa ada ya euro milioni 24 mnamo Septemba, na tayari ameshawavutia miamba wa LaLiga –Barcelona.

Fowadi huyo wa miaka 21 alianza vyema kwa hat-trick kwenye Ligi ya Uropa mwezi uliopita, wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay akiwa na mabao matano kwenye mashindano yote.

Juventus pia wamehusishwa na Nunez, lakini Benifca walipoulizwa juu ya hatma ya mshambuliaji huyo, kupitia Lasalvia walisema “Darwin atabaki Benfica angalau hadi 2022.”

 

Darwin Nunez To Barcelona
NUnez

Kocha mkuu wa Benfica, Jorge Jesus anatarajia Nunez kumzidi Joao Felix kuuzwa kama mchezaji ghali zaidi wa kilabu. Barcelona wajipange kuinasa saini yake.

Joao Felix aliondoka Benfica kwenda Atletico Madrid kwa rekodi ya kilabu milioni 126 mwaka jana.

“Tuko sawa. Hatupaswi kusahau kuwa yeye ni mtoto, ana umri wa miaka 21, kuna mengi juu ya mchezo ambao bado hajui. Atajifunza kutoka kwangu na Benfica,” Jesus alinukuliwa na  SportTV.

Benfica waliruhusu kichapo cha 3-2 dhidi ya Braga Jumapili kwenye mechi ya Primeira Liga. Matokeo hayo yameiacha Benfica ikiwa nyuma kwa alama nne dhidi ya viongozi na wapinzani Sporting CP.


 

Umejaribu hii Poker ya Video?

Jaribu sasa hapa Meridianbet, ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

Ingia mchezoni!

23 MAONI

  1. Barcelona imekuwa na wakati mgumu sana hivi karibuni. Haina fedha na haina wachezaji mahili wanaoweza kuleta matokeo mazuri uwanjani na kwabahati mbaya inanunua wachezaji wasioendana na falsafa yao

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa