Barcelona hatimaye wamekamilisha usajili wa kiungo Jules Kounde baada ya klabu kukosa fedha za mikataba mingine na kumtoa kwa mkopo Samuel Umtiti.

Jules Kounde yuko huru kuichezea Barcelona baada ya kuthibitishwa kusajiliwa na La Liga
Pesa zilizoachiliwa kutoka kwa kandarasi za wachezaji na mkopo wa Samuel Umtiti zilisaidia kupata pesa za usajili wa mchezaji huyo.

barcelona, Barcelona Yamsajili Jules Kounde LaLiga., Meridianbet

Kulingana na ripoti ya The Athletic, iliandika kuwa usajili wa majira ya kiangazi utapatikana kwa vijana wa Xavi kabla ya mechi yao na Real Valladolid siku ya Jumapili.

Barcelona iliishinda Chelsea katika usajili wa kiungo huyo, na alikuwa mchezaji wa mwisho kuletwa kwenye klabu msimu huu wa kiangazi ambaye alishindwa kuongezwa kwenye kikosi chao cha La Liga. Lakini Inashangaza kwamba Kounde alivaa jezi ya zamani ya Umititi nambari 23 katika mechi mbili za kirafiki za hivi majuzi dhidi ya Pumas na mechi ya katikati ya wiki dhidi ya Manchester City licha ya kuwa bado hajasajiliwa na klabu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa