Barry Geraghty ameamua kufungua ukurasa mpya wa maisha yake baada ya kuamua kustaafu mbio za farasi akiwa na miaka 40.

Barry ametumia kurasa yake ya twitter jumamosi jioni kudhibitisha kustaafu kazi yake aliyoitumikia kwa miaka 24.

 

Barry Geraghty Astaafu Mbio za Farasi.

 

Geraghty ameshinda karibu mbio zote kubwa ikiwemo Grand National aboard Monty Pass mwaka 2003 na Ushindi wa kishindo wa mara 43 katika Mashindano ya Mbio za Cheltenham.

Geraghty anahisi majeraha yamepelekea kufanya maamuzi ya kustaafu katika Ulimwengu wa Mbio za farasi (Jockey).

“Nitakuwa na miaka 41 mwezi wa tisa, na siwezi kuendelea kucheza kucheza maisha yote.

“Nimekua majeruhi kwa miezi 18 ndani ya miaka 5 iliyopita baada ya kuvunjika miguu yote, mikono yote, mbavu zangu, bega na maumivu mengine ni moja ya majeruhi hayo.

“Mbavu nane zilivinjuka na kupelekea kuumia mapafu hivyo kufanya nikose mashindano ya Cheltenham mwaka 2017, pia kuvunjika kwa mkono katika mashindano ya Fairyhouse mwezi wa nne siku 11 baada ya kutoka kwenye majeraha ya kuvunjika mbavu, yalikua moja ya majeraha mabaya katika wakati mbaya.

“Majeraha yangu ya mwisho ilikua ni kuvunjika mguu mwaka 2019 katika mashindano ya Grand National pale Aintree, Ilikua ni jaribu kubwa na gumu kulipokea.”


Jiunge na meridianbet kufurahia Michezo kibao.

Jiunge Hapa.

45 MAONI

  1. Ndio wakati muaafaka wa kistafu maana ameshiliki kwa muda mrefu sanaa na amepata mafanikio makubwa kwenye haya mashindano

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa