Raisi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amesisitiza kuwa Lionel Messi alishasema kuwa anataka kustaafu kalabuni hapo. Bartomeu amezungumzia hili kufuatia tetesi za Messi kutaka kuondoka klabuni hapo.

Taarifa zilizovuma zaidi wiki iliyopita na mwishoni mwa mezi Mei ni kuwa kuna baadhi ya mambo yamemchosha Messi. Hivyo mpango wake wa sasa ni kuondoka klabuni hapo.

Mshindi huyu wa mara 6 wa Ballon d’Or amesaini mkataba na Barcelona hadi 2021. Kufuatia hali ya uhusiano wake na klabu, ripoti nyingi hasa za Alhamisi zilitaja kuwa anafikiria kuondoka. Wakati huo klabu za PSG na Man United zikitajwa kama klabu zilizokaa chonjo kuinasa saini yake.

Lionel Messi amekuwa akitoa mchango mkubwa kwa Barcelona kwa mda mrefu. Wajuzi wa mambo huwa wanatania kuwa Messi akiondoka, basi anasepa na sifa za Barcelona. Hapa ina maana Barca watakuwa kama nyuki wa mashineni pale La Liga. Kwako imekaaje hii?\

Messi alikataa kusaini mkataba wa maisha Barcelona

Raisi Bartomeu  alivyoulizwa, hakutaka kuzungumzia hili moja kwa moja. Kwa kifupi alisema kuna mazungumzi yanaendelea na wachezaji wengi. Alisitiza kuwa hawezi kuwa anatoa taarifa kila siku za kinachoendelea au mchezaji mmoja mmoja.

“Siwezi kuelezea kwa undani kile kinachoendelea kila wiki. Kuna mazungumzo na wachezaji wengi. Kwa Messi yeye alishasema kuwa anataka kustaafu Barcelona.”

-Josep Maria Bartomeu

Inakumbukwa kuwa klabu ilikuwa tayari kumpa Messi mkataba wa Maisha. Lakini staa huyu alikataa ofa ya mkataba huo kwa kuwa alikuwa hataki kujifunga kuja kufanya maamuzi tofauti baadaye. Lakini kwa sasa kuna sintofahamu juu ya hatma yake.

 


Unajua kuwa Meridianbet wanatoa mizunguko 50 ya bure kwa mteja mpya? Jisajili sasa na ufurahie burudani na ushindi wa Kasino ya Mtandaoni.

JISAJILI HAPA

Mizunguko ya Bure | Kasino ya Mtandaoni

52 MAONI

  1. Hizo n habar za magazeti na tetesi tuu kwa vyombo vya habar ila messi hawezi kuondoka pale Barcelona mpira wake atamalizia pale mimi sion mtu wa kuondoka pale labda wachezaji wengine ila sio messi

  2. Kama vipi ahame timu ili heshima take ibaki vilevile pale Barcelona na hispania kwa ujumla ili aje kujumbukwa baadaye

  3. Messi ni mchezaji wa Barcelona hadi hapo atakapo maliza career yake ya mpira istoshe messi mwenyewe anaipenda Barcelona ile kutoka moyoni ukitupilia mbali tu Kama ni sehemu yake ya kazi damu ya messi ni Barcelona tupu.

  4. Messi ana miaka 33, kustaafu akiwa Barcelona ni heshima kwake na endapo ataamua kuondoka timu itayumba kwa muda fulani kwasasa imejengwa kutokana uwepo wake#meridianbettz

  5. Messi akiondoka Barcelona itakuwa kwny wakati mgumu sna ila kweli umri umeenda San sio mbaya akistaafu soka

  6. Ipo wazi hii Messi hawezi toka barca na kwenda kucheza timu nyingine mpaka kustaafu soka inajulikana hii yeye ni kama mfalme pale barca

  7. Messi mwenyewe alishasema kuwa atastaafu soka akiwa kwenye timu yake Bacerlona kwahiyo hao wengine wanajisumbua tu ,Messi ni Bacerlona damu

  8. Mwache tu astafie hapo hapo maana kwa tetesi hata wakimchukua man u hatoweza kabisa kucheza pale… Ni bora Tu abaki pale maana hata time yake ya Argentina inamshinda..

  9. Lionel Messi amekuwa akitoa mchango mkubwa kwa Barcelona kwa mda mrefu. Wajuzi wa mambo huwa wanatania kuwa Messi akiondoka, basi anasepa na sifa za Barcelona.

  10. Hayo ni maneno ya waandishi ambao wanataka kupata umaarufu katika kazi zao ili ikuwe kirahisi sisi tunataka ahame kabisa au aendelee kubaki mana tumeshasikia Mara kwa Mara kuhama kwake lakini hatuoni kuhama kwake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa